tiko
tiko
Jumla
ya mashabiki 40,000 walihudhuria kwenye dimba la nyumbani la klabu ya
Atletico Madrid la Vicente Carderon kumlaki kwa mara ya pili shujaa wao
wa miaka mingi aliyekua ametimukia ughaibuni Muhispania Fernando
Torres.
Jambo
hili linaweza likawa la ajabu sana miongoni mwa mashabiki wa klabu ya
Chelsea lakini walichokifanya mashabiki wa klabu ya Atletiko ni kuonesha
kiasi cha upendo walichonacho kwa Muhispania mwenzao ambaye wanamuona
kama amegeuzwa mbuzi wa kafara na klabu ya Chelsea.
Torres,
alijitengenezea jina kubwa sana alipokua akiitumikia klabu hiyo pale
ambapo alipofanikiwa kuifungia jumla ya magoli 82 kwenye michezo
takribani 214.
Hii
ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo kurejea Vicente Calderon tangu
mwaka 2007 na huenda akapata faraja kubwa kutokana na mapokezi ya
kishujaa aliyoyapokea kutoka kwa mashabiki hao.
tiko
tiko
Post a Comment