tiko
tiko
Manchester United imeuanza mwaka 2015 kwa matokeo ya sare baada ya kutoka suluhu ya 1-1 katika mchezo wao wa 19 wa ligi kuu ya England dhidi ya Stoke City uliopigwa kwenye uwanja wa Brittania .
United waliuanza mchezo huo vibaya baada ya kujikuta wakiwa nyuma kwenye dakika ya pili tu ya mchezo baada ya kuruhusu bao lililofungwa na beki wao wa zamani Ryan Shawcross ambaye alimalizia pasi ya Peter Crouch baada ya mpira wa kona uliopigwa na Stoke .
United walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 26 ya mchezo mfungaji akiwa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao ambaye aliugusa kidogo mpira ulioanzia kwa Waybne Rooney ukipitia kwa Juan Mata .
Mchezo huo haukuwa na purukushani nyingi hali iliyosababisha makipa wa pande zote mbili kuwa nje ya mchezo kwa muda mrefu japo Stoke wangeweza kushinda baada ya kunyimwa penati ya wazi huku mshambuliaji Peter Crouch akigonga mwamba katika moja ya mashambulizi machache kwenye mchezo huo .
Matokeo haya yanawafanya United washindwe kuwasogelea Manchester City walio kwenye nafasi ya pili huku wao wakisalia kwenye nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 37 huku Stoke City nao wakiendelea kubaki kwneye nafasi ya 11 wakiwa na jumla ya pointi 26 .
Radamel Falcao akiutazama mpira wake ukitinga kwneye wavu wa Stoke City huku kipa Asmir Begovic
tiko
tiko
Post a Comment