tiko
tiko
MUIGIZAJI mkongwe
nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa wa filamu Bongo
kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.Muigizaji mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’.
Akizungumza na Uwazi, Mama Abdul
aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuisha kwa uzinduzi wa kitabu hicho
uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Landmark,
Ubungo Riverside ambapo alisikitishwa kutokana na marehemu kuwa mchango
mkubwa katika tasnia ya filamu.
“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi
jeuri ya kumtenga Mama Kanumba wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au
tuseme wameona kwenye uzinduzi hakuna namna ya kupiga dili kama
walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia sura.”Mama Kanumba( wa tatu kulia) akiwa na wadau waliojitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.
“Wamenikera, halafu wakimuona Mama
Kanumba wanajifanya kumsalimia kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba
waache kujishauwa,” alisema Mama Abdul.
tiko
tiko
Post a Comment