tiko
tiko
Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka
Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka
$56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa
mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli
za usafiri wa umma kupungua.
Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya
mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni
karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.
EWURA, inasemekana, wamesema kuwa bei za
hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa
ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei.
Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka
mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei
ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua
' bulky' huwa hazitolewi.
Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta
yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji
hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri
lazima bei za pampu zipungue.
Vile vile ni kweli kwamba thamani ya
shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa
bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa
Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati
shilingi imeshuka kwa chini ya 10%.
Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.
Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA
wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana
na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia.
Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.
Zitto Kabwe, Mb
Zitto Kabwe, Mb
tiko
tiko
Post a Comment