tiko
tiko
Baba wa nguli wa filamu Bongo, marehemu
Steven Charles Kanumba, Charles Kanumba, amesema kuwa anaamini kama
mwanaye angekuwa hai hadi sasa basi angekuwa mwanasiasa maarufu nchini
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa
kijijini kwao Shinyanga, Charles alisema, japo imepita miaka kadhaa
tangu kutokea kwa kifo cha mwanaye huyo, bado anawaza ni namna gani
angeweza kuleta maendeleo kwa Watanzania.
“Mwanangu alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa
mwanasiasa tena kwa kupitia tiketi ya CHADEMA. Alikuwa akinieleza mambo
mengi ya kisiasa lakini kwa bahati mbaya Mungu alimchukua,” alisema
Charles.
tiko
tiko
Post a Comment