tiko
tiko
Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam iko mbioni kuingia mkataba kocha mpya kutoka Serbia baada ya kumalizana na kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye alifukuzwa kazi siku chache zilizopita.
Kocha huyo Goran Kapunovic
aliingia nchini Tanzania akitua kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere hapo jana saa 1 asubuhi na alikuja kupokewa na
viongozi wa Simba akiwemo mjumbe wa timu hiyo Colin Firsch.
Simba ilimfukuza Phiri mapema wiki hii
baada ya klabu hiyo kutoridhika na kiwango cha timu hiyo kufuatia
mfululizo wa matokeo mabaya hasa kwenye mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya
Kagera Sugar ambapo wekundu wa msimbazi walifungwa 1-0.
Simba kwa sasa iko visiwani Zanzibar
ambako inashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi huku ikiwa chini ya
kocha msaidizi wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye ataiongoza timu hiyo hadi hapo kocha mpya atakapoungana rasmi na kikosi chao.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichomo ndani ya klabu hiyo ambacho hakikuwa tayari kunukuliwa Phiri tayari ameagana na wachezaji wa timu hiyo baada ya maamuzi ya kuachana nae.
Kocha huyo mpya ni raia wa Serbia na aliwahi kucheza kwenye michuano mikubwa ya ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na timu ya Ferencvaros ya nchini Hungary na mara ya mwisho alikuwa amefundisha klabu ya Polisi ya huko Rwanda.
Simba itaingia uwanjani usiku wa leo kucheza mechi yake ya kwanza ya
kombe la mapinduzi dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Amaan
visiwani Zanzibar.
tiko
tiko
Post a Comment