tiko
tiko
Siku za Fernando Torres kutambulishwa kama mshambuliaji wa Ac Milan na Chelsea zinazidi kukaribia kufikia mwisho baada ya usajili wa mchezaji huyo ndani ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid kukamilika .
Tayari makubaliano baina ya pande zote zinazohusika yamefikiwa na kilichobaki na kwa mikataba rasmi kutiwa saini na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia tarehe 30 ya mwezi huu Torres ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Diego Simeone.
Usajili wa Torres ulianza kuiva baada ya klabu inayommiliki ya Chelsea kukubali kumruhusu mchezaji kuondoka bure hali iliyomfanya awe mchezaji kamili wa Ac Milan ambayo kwa upande wake ilikubali kumbadili na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Alesio Cerci ambaye anacheza Atletico Madrid.
Habari toka huko nchini Hispania zinasema kuwa wawakilishi wa pande zote zinazohusika kwenye makubaliano haya walikutana siku ya jumamosi na ufanya mazungumzo ambayo yaliashiria makubaliano ya msingi juu ya usajili wa wachezaji hawa wawili (Torres na Cerci ) na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia jumanne (Dec 30) Torres atatambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Atletico Madrid.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Fernando Torres kufanya kazi na Diego Simeone baada ya wawili hawa kuwa pamoja kama wachezaji katika miaka ya 2000 wakati Torres alipokuwa anaanza maisha yake kama mshambuliaji chipukizi kwenye kikosi cha Atletico Madrid .
tiko
tiko
Post a Comment