tiko
tiko
MWIGIZAJI Ndumbagwe Misayo maarufu kama
Thea, amesema wasanii huvaa sketi fupi ‘vimini’ wakilenga kwenda na
wakati na si kujipitisha mbele ya wanaume.
Thea aliiambia Mwanaspoti, kuwa ni kama
wanatekeleza wimbo wa mwanamuziki Bwana Misosi ‘Nitoke Vipi’, lakini
haimaanishi kwamba wavaaji wote ni wahuni.
“Vimini ni ‘kiki’ tu mjini, watu wengi
wanaamini ni sehemu mojawapo ya uvaaji au Nitoke Vipi kama Bwana Misosi
alivyosema. Kuna watu wanaamini waigizaji tunaovaa au wanaovaa vimini
wanafanya hivyo ili kutafuta biashara, ukweli ni kwamba hakuna kitu kama
hicho, kama wapo basi ni kumi kwa mmoja,” alisema Thea.
“Vimini ni ‘kiki’ tu ya mjini. Watu
wanaweza kununua filamu kwa sababu wanataka kuona paja la mtu Fulani.
Hapo unakuwa umeuza filamu si mwili.”
tiko
tiko
Post a Comment