tiko
tiko
TUKIWA tunaelekea
ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’
amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa hauna bahati (gundu) hivyo anamuomba
Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake.
Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akipiga stori na gazeti hili, Dude
alisema ndani ya mwaka huu hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya
yale aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo
linamuumiza kwani alitegemea kufanya mambo mengi lakini hakufanikisha
“Nilitegemea kufunga ndoa lakini
imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia
nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani
lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu
namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.
tiko
tiko
Post a Comment