tiko
tiko
Mwaka
hauishi vizuri kwa Raia wa Marekani ambao wana asili ya Afrika, ile
story ya ubaguzi ambayo huenda Dunia ilidhani imekwisha imechukua sura
mpya kila kunapokucha, kinachosababisha story kuwa kubwa zaidi ni
kitendo cha hali hiyo kujitokeza ndani ya Taifa la Marekani.
Tumeona Marekani ikiwa mstari wa mbele kupambana na vingi, hii ishu ya ubaguzi wa rangi ni changamoto kubwa taifa hilo kwa sasa.
Wameuawa wengi tayari ndani ya kipindi
kifupi, watu hao wenye asili ya Afrika wameandamana na kutumia njia
mbalimbali kuonyesha hawakuridhishwa na Mahakama kuwaachia huru Askari
ambao wamefanya mauaji hayo.
Kutokana na matukio hayo ya mauaji kuendelea kujitokeza rapper 50 Cent, ameamua kuvunja ukimya na kujitokeza kuelezea kukasirishwa kwake na matukio hayo ya mauaji na kupost picha ya Hayati Mahatma Gandhi iliyoandikwa “An eye for an eye makes the whole world blind“.
Kisha akaandika ujumbe wa kuwafariji waliopata athari kutokana na tukio hilo; “Condolences
to the family of the 2 officers.RIP Mike Brown, RIP Eric Garner
randomly shooting police officers is not the answer. Mayor De Blasio get
your a** to work!!!! #SMSAUDIO #POWERTV #FRIGO#EFFENvodka”– @50cent
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment