tiko
tiko
WIKI
iliyopita tuliishia pale ambapo staa wa Bongo Fleva, Diamond aliachia
video yake ya Number One katika uzinduzi usiyo na kiingilio alioufanya
ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo pia alimzawadia gari,
aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.
Wiki hii tunaendelea ambapo katika kuanika maisha yake, Diamond anasema:

ASIFU KAMPANI YA DAVIDO
“Mwezi wa 10, 2013 nilifanya kolabo na Davido (David Adedeji Adeleke) kutoka nchini Nigeria katika video ya Number One remix halafu nilifunga safari hadi Nigeria lengo likiwa ni kuangalia masoko ya muziki katika nchi za wenzetu.

“Naweza kusema wimbo wa Number One ndiyo
uliweza kunitambulisha kimataifa, nilipata mashabiki kibao na
kushiriki kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo MTV Mama nchini Afrika Kusini
ambapo nilipanda jukwaani na Davido. Kuna tuzo nyingine kama BET,
Afrimama, MTV Europe Channel O,” alisema Diamond.
Julai 7, mwaka huu, Diamonnd alimzawadia
gari mama yake aina ya Toyota Lexus pia aliachia video mbili za
Mdogomdogo iliyofanyika nchini Uingereza na Bumbum aliyomshirikisha
Iyanya kutoka Nigeria aliyoifanyia Afrika Kusini. Video hizi anasema
zilimgharimu dola 78,000 za Marekani.
KUTUA DAR LIVE KRISMASI
Hivi karibuni, Diamond alikuwa nchini Uganda kwenye shoo ya nguvu ya mwanamuziki wa nchi hiyo, Zarina Hassan ‘Zari’ lakini amerudi Bongo haraka sana kwa sababu keshokutwa (Alhamisi) anapanda kwenye jukwaa la Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem kwa ajili ya kutoa raha ya Sikukuu ya Krismasi.

Diamond atapanda na Mzee Yusuf wa Kundi la Jahazi Modern Taarab.
Anaitwa Diamond Platnumz, mzaliwa wa Kitongoji cha Tandale kwenye Jiji la Dar es Salaam, ameweza kukitumia kipaji chake vizuri na kupata mafanikio makubwa sana. Hongera sana Diamond.

Post a Comment