tiko
tiko
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa
utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola
utafanyiwa kazi mapema mwakani.
Dar es Salaam. Wenyeviti watatu wa Kamati za
Bunge waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la
Akaunti ya Tegeta Escrow wataondolewa katika nyadhifa zao ndani ya siku
21 zijazo, imeelezwa.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa
utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola
utafanyiwa kazi mapema mwakani.
“Hilo litatekelezwa wakati wa Kamati za Bunge
ambazo zitaanza mwishoni mwa wiki ya pili ya Januari mwakani kwa kamati
husika kuchagua wenyeviti wapya.”
Wenyeviti hao ni wa Kamati ya Nishati na Madini,
Victor Mwambalaswa, William Ngeleja wa Katiba, Sheria na Utawala na
Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti.
Tuhuma zao
Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM)
alitajwa katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
kuwa aliwekewa Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kama ilivyokuwa
kwa Ngejela (Sengerema -CCM) ambaye aliingiziwa Sh40.4 milioni. Wote
waliingiziwa fedha hizo na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering &
Marketing, James Rugemalira.
Mwambalaswa, ambaye pia ni Mbunge wa Lupa (CCM),
ametajwa kwa kuwa alikuwa makamu mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco ambayo
Bunge liliazimia kuwa wajumbe wake wawajibishwe.
Katika azimio namba tatu, Bunge lilielekeza kuwa
kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa
vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao
wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.
Utekelezaji wa azimio hilo unakuja baada ya Serikali kuanza kuwawajibisha vigogo wake waliotajwa katika ripoti hiyo.
Jumatatu iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimfukuza
kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka ambaye kama ilivyokuwa kwa Chenge na Ngeleja, aliingiziwa
Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kinyume na kanuni za maadili
ya viongozi wa umma.
Pia, wakati Rais Kikwete akimuweka kiporo Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, juzi Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi
yake.
Hao wote walitanguliwa na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa
hiyo akisema ushauri wake haukueleweka hivyo kuchafua hali ya hewa.
CHANZO; MWANANCHI.
CHANZO; MWANANCHI.
tiko
tiko
Post a Comment