tiko
tiko
BAADA ya
wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye
moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo
Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea
kuibuka.
Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara
anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye
mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha
shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara.
Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa
yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza kuishi na mwingine kwani
wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa
sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari
na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni
kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe ya kipekee na zoezi hili
tutalifanya mwakani,” alisema.
tiko
tiko
Post a Comment