tiko
tiko
Picha aliyoweka Faiza Ally Instagram ya Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akiwa katika pozi na mwanaye Sasha.
MSANII wa filamu Faiza Ally ambaye
amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo amewatolea
uvuvi watu waliokuwa wakijiuliza maswali kuhusu mwanaye Sasha na na baba
yake.
Kupita akaunti yake ya Instagram, Faiza
ameweka picha na Mhe. Sugu akiwa na mwanaye Sasha na kuandika kuwa
"Mara nyingi huwa nawapiga picha mimi mwenyewe sema tu sipendi sana
kurusha kwangu"
Na kwa wale waliokuwa wanauliza maswali
juu yao, Faiza amewajibu hivi: "Ni kweli kuna wakati tulikuwa
hatuelewani kabisa na wala hatukuwa tunaonana lakini kwa sasa tofauti
zetu zimeisha hatuna ugomvi japo hatuko pamoja"

Faiza akiwa na Mhe. Sugu enzi hizo.
"Lakini mwisho wa siku huyo ndiyo baba
Sasha na mzazi siku zote atakuwa mzazi tu, haijalishi tuna tofauti kiasi
gani" Alimalizia kuandika msanii huyo asiyeishiwa vituko.
Baada ya kuwek picha hiyo wengi wa
mashabiki wa Faiza walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wakiwataka
warudiane ili walee mtoto pamoja.
tiko
tiko

Post a Comment