Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

YALIYOJILI BUNGENI

tiko tiko
Fredrik Werema amekubali rasmi kung'atuka katika cheo hicho baada ya ripoti ya PAC kuwekwa rasmi hadharani huku waziri mkuu Mizengo Pinda akisema anasubiri hatma yake katika majadiliano yatakayofanyika bungeni, nimethibitisha.

Aidha waziri prof. Anna Tibaijuka naye amekubali kung'atuka baada ya ripoti ya PAC kusomwa bungeni.

Hayo yameamuliwa katika kikao cha CCM chini ya Philip Mangula kilichomalizika mjini Dodoma leo alfajiri.

Pinda amesema kuwa hatma yake iko mikononi mwa wabunge kama watapitisha kwa kauli moja kuwa ang'atuke yupo tayari kufanya hivyo

kutokana na ripoti ya PAC kutokumuwajibisha kwa lolote lile.

Ripoti ya PAC imewawajibisha kwa uzembe AG Werema, Saad Mkuya-fedha, Muhongo Sospeter- Nishati na madini na gavana Beno Ndulu.Aidha wengine ni vigogo wote wa juu wa Tanesco.

Kwa upande mwingine bunge limeambiwa liamue hatma ya waziri mkuu pamoja na mawaziri wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu huku wakikwepa sekeseke la kuwajibishwa na PAC.

Kikwete anatarajiwa kurejea kesho usiku ambapo atalazimika kumteua AG mpya na kulisuka upya baraza la mawaziri na kama wabunge wataamua kumsulubu Pinda( kutokana na utashi wao kwani hajabanwa na PAC) basi Kikwete atalazimika kuiunda upya serikali.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top