Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

MLEVI MMOJA

tiko tiko
Mlevi mmoja alikuwa na tabia ya kwenda bar,
kisha anaagiza bia moja na grass mbili za
kunywea, anajaza bia kwenye grass zote mbili
kisha anakunywa moja baada ya nyingine.Siku
moja muhudumu aliamua kumuuliza kwa nini
alikuwa akifanya vile, jamaa akajibu '' unajua
kipindi cha nyuma nilikuwa nikija bar na kunywa
na rafiki yangu kipenzi ambaye kwa sasa ni
marehem, hivyo nafanya hivi kwa lengo la
kumuhenzi rafiki yangu kipenzi, yaani grass moja
yangu, na nyingine ni kwa ajili yake'' Duh!!!
muhudumu alishangaa sana. Siku moja yule mlevi
alikwenda bar kama kawaida yake, alipofika
akaagiza bia na grass moja, muhudumu
akamuuliza leo vip mwenzetu mbona grass moja?
jamaa akajibu ''Unajua mimi leo ni siku ya tatu
tangu nimeacha kutumia bia, lakini kwa kuwa rafiki
yangu alifariki ajaacha kunywa, nimeona sio mbaya
kuendelea kumuhenzi, ndo mana leo nimeagiza
grass moja kwa ajili ya rafiki yangu''
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top